Habari ndugu mwanchama wa TFDA Workers SACCOS Ltd, Natumaini unaendelea vizuri na majukumu yako ya kila siku.
Napenda kukukaribisha kwenye Moduli ya 3 ya Program yetu maalum kuhusu JINSI YA KUJENGA TABIA YA KUWEKA AKIBA KWA HIARI KUPITIA SACCOS anbayo inalenga kukuza mtaji wa chama ili kuongeza uwezo wa SACCOS kuboresha zaidi kasi ya utoaji mikopo kwa wanachama wake.
Moduli hii ni ya muhimu sana kwa kuwa inahusu kuchukua hatua. Hivyo, unaombwa utenge muda wa kutosha kupitia moduli hii.
Matarajio yetu ni kwamba umekamilisha kupitia mada zote za Moduli ya kwanza na ya pili ambazo tumekua tukizitoa kupitia video za kwenye you tube.
KAMA JIBU NI NDIO HONGERA SANA. SASA KAMILISHA SAFARI YAKO KWA KUANGALIA VIDEO ZILIZOPO KWENYE MODULI 3 KWA KUFUATA MAELEZO YALIPO KWENYE KILA VIDEO
MODULI YA 3: KUCHUKUA HATUA
Kwenye moduli hii tumedhamiria wewe kama mdau muhimu katika programu hii uweze kufanya mambo makubwa 4 kama ifuatavyo:-
- Kuwa na uelewa wa pamoja sababu zilizofanya SACCOS iandae Mpango wa Kuongeza Mtaji;
- Utambue maalengo ya Mpango huo;
- Mikakati na Dhana iliyotumika katika kuweka mikakati; na
- Hatimaye uchukue hatua ya kuongeza kiasi cha akiba yako ya kila mwezi.
Vido 1: Sababu 2 za SACCOS kuja na Mpango wa Kukuza Mtaji wa Chama
Video 2: Tambua mikakati iliyowekwa ili kufikia malengo
Video 3: Pakua Kikokotoo cha kukadiria kiasi cha akiba ya kuongeza
Karibu sasa uanze kuchukua hatua kwa kuanza na kukadiria kiasi cha akiba unachopaswa kuongeza. Kubaini kiasi hicho tafadhali bofya alama ya play iliyopo kwenye video hii.
BOFYA HAPA SASA KUPAKUA KIKOKOTOO CHA KIASI CHA AKIBA YA KUONGEZA

No comments:
Post a Comment